August 17, 2020

 


KLABU ya Yanga kwa sasa kwenye dirisha la usajili lililofunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31 wameshamalizana na majembe saba ya ndani kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.


Hii hapa orodha kamili ya wachezaji wazawa ambao wameshamalizana na Yanga watakipiga msimu wa 2020/21 na tayari timu inaendelea na mazoezi pale Uwanja wa Chuo cha Sheria,:- 

Farid Musa yeye ni kiungo mshambuliaji alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya CD Tennerife ya Hispania na mkataba wake ulikuwa umekwisha.

 Yasin Mustafa  yeye ni beki wa kushoto alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania.

 Zawadi Mauya anacheza nafasi ya kiungo mkabaji alikuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar.

 Bakari Nondo Mwamnyeto yeye ni beki wa kati alikuwa anakipiga ndani ya Coastal Union.

 Abdalah Shaibu  yeye ni beki wa kati alikuwa anakipiga ndani ya MFK Czech ya Serbia.

 Kibwana Shomari  yeye ni beki wa kulia alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar.

 Waziri Junior yeye ni mshambuliaji alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mbao FC.

Nyota hao wote wamesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga.

4 COMMENTS:

  1. kwani sisi hatujui kama huna cha kuandika nyamaza tu maana ni ujinga mtupu

    ReplyDelete
  2. Kasahau kasema usajili wa Yanga badala ya kusema usajili wa Mabingwa Wa Jadi kama ilivo siku zote, jambo ambalo kaiteremshia hadhi yake

    ReplyDelete
  3. Jaman yan kila kitu nikujaji tuuuu

    ReplyDelete
  4. Yaan aisee hata me nashangaa kwa kweli kila kitu mnajaji tu bas mpeleken mahakamani.....Salehjembe mwanangu lete vitu tusome asietaka asifungue

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic