MKURUGENZI Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said, ametaja majukumu atakayoyafanya aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Senzo asaini mkataba wa kufanyakazi na Yanga mara baada ya kuachana na Simba.
Hersi ameliambia Spoti Xtra kuwa, Senzo ametua hapo kusaidia kusimamia mabadiliko ya utawala ndani ya klabu hiyo na siyo kuwa mtendaji mkuu.
Aliongeza kuwa, ni ngumu kwa Senzo kuwa mtendaji mkuu wa Yanga kutokana na katiba kutoruhusu kiongozi wa kigeni kufanya majukumu hayo makubwa.
Yanga hivi sasa ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kukamilisha mfumo wa mabadiliko wa uongozi ambapo hivi karibuni waliingia makubaliano na La Liga waliopewa jukumu la kusimamia zoezi hilo.
“Senzo anakuja kusimama katika kusaidiana na uongozi kwenye mabadiliko ya utawala ambayo tayari ungozi wameuanza kwa kushirikiana na GSM ambao ndiyo wanaosimamia kufanikisha zoezi hilo.
“Kwa hivi sasa hawezi kuwa ofisa mtendaji mkuu kwa kuwa katiba ya klabu hairuhusu kiongozi kama huyo raia wa kigeni kuja kupewa jukumu hilo.
“Mara baada ya mchakato huu wa mfumo wa mabadiliko wa uongozi wa Yanga utakapokamilika ndiyo anaweza akachukua nafasi hiyo ya utendaji,” alisema Hersi Said.
Katika hatua nyingine, inaelezwa kuwa Senzo Jumatatu jioni alienda Simba na kukabidhi ofisi na vifaa vyote vya klabu hiyo ikiwemo gari aina ya 2020 Mercedes-Benz alilopewa na mwekezaji wa klabu hiyo, bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Wakati huohuo, uongozi wa Simba umesema itakuwa ngumu hivi sasa Senzo kuanza kazi ndani ya Yanga kwa kuwa kibali chake cha kazi kinamtambulisha kuwa ni mali ya Simba.
Crescentius Magori aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba kabla ya nafasi yake haijachukuliwa na Senzo, amesema: “Utaratibu upo wazi, nilishangaa kuona mtendaji mkubwa kama yeye anashindwa kufuata weledi na kuibukia kwenye mitandao ya kijamii, lakini ukweli ni kwamba hawezi kuanza kufanya kazi huko alikokwenda mpaka watakapokuja mezani kuzungumza nasi.
“Kibali cha kazi kwa sasa kinaonyesha kuwa yeye ni mfanyakazi wa Simba, lazima tuthibitishe kwa kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani alikopewa kibali kisha tumruhusu aende huko anakotaka, hii haina ujanja ni utaratibu tu lazima Yanga waje tuwape kibali ili aanze kazi kwao.”
Kibali kitatoka tu, hayo ni majibu ya jazba.
ReplyDeletePia kama niutaratibu basi hata kibali cha Morrison kipo Yanga...
Manyani katika ubora wao
ReplyDeleteMagori amechemka katika hili la kusema "walipata kibali cha kumruhusu Senzo kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani!!" Inatambulika wazi kuwa kibali cha ruhusa ya kufanya kazi hapa nchini kwa raia wa kigeni hutolewa na wizara ya kazi au labda kuna utaratibu mpya? Bali visa ndio hutambulisha mgeni huyo ni mtembezi, mtalii au mtaalamu.
ReplyDeleteAidha kama amesema hivyo basi tutambue hao ndio aina ya viongozi wa hizi klabu zetu!! La si hivyo basi mwandika habari ndio tatizo.
Magori hajasema kuwa "walipata kibali cha kumruhusu Senzo kufanya kazi wizara ya mambo ya ndani", bali alichosema ni Kibali cha kazi kwa sasa kinaonyesha kuwa yeye ni mfanyakazi wa Simba, lazima tuthibitishe kwa kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani alikopewa kibali kisha tumruhusu aende huko anakotaka, hii haina ujanja ni utaratibu tu lazima Yanga waje tuwape kibali ili aanze kazi kwao.”angalieni vitu vinginre mnavyoandika usikurupuke tu kusema Magoli anachemka
DeleteWizara ya mambo ya ndani kupitia Idara ya uhamiaji ndio final wa kuidhinisha 'work permit'ya non-citzen anayeajiriwa kufanya kazi nchini ilihali mtiririko wa kibali cha kazi kinaanzia wizara ya kazi na kawaida muajiri ni lazima aitangaze hiyo kazi ili kama kuna mtanzania mwenye sifa na vigezo za kufanya hiyo kazi ndio anapewa kipaumbele cha kuajiriwa na akikosekana basi mgeni mwenye sifa anapewa hiyo kazi.Sheria hizi sio mpya, zilikuwepo na bado hazijabadilishwa lkn ni kama tunajifanya hazipo angalau awamu hii ya tano ya utawala inajitahidi kulidhibiti kwa wageni kufanya kazi nchini kiholela na bila kuwa na sifa stahiki.
DeleteKuntu
DeleteHivi viongozi wa Yanga mbona hawaongei. Kila siku ni Hersi tu. Msola amepinduliwa??
ReplyDeleteUsajili Hersi, kesi Hersi, Senzo Hersi, habari Hersi. Huyu ni mmiliki wa Yanga??
Hayakuhusu!
DeleteWenye akili zetu tulijua tu uongozi wa Yanga hawakuwa wanamuhitaji Senzo Masingisa wakati huu ila Senzo katumika na ataendelea kutimika wakati huu viongozi wa Yanga kujaribu kufunika uozo na ubabaishaji na udanganyifu kwenye usajili wa Morrisoni na inaonekana so far viongozi wa Yanga wamefsnikiwa kuwalaghai Mashabiki wao tena, ila wahenga wa waswahili wana msemo usemao njia ya amnafiki fupi kwa maana yakwamba uongo au unafiki haudumu kabla ya ukweli kujilikana.Mafanikio ya kweli hayana njia ya mkato yana taratibu zake na hapa ndipo watanzania tunapofeli. Tujifunze tu kwa simba ingawa hawajafika kileleni ila unaona kabisa wanavyokwenda hatua kwa hatua kutoka mikutano ya wanachama wao kuidhinisha mabadiliko ya katiba ya uendeshaji wa timu yao hadi zoezi la kusajili wanachama wao nchi nzima mpaka kumiliki viwanja vyao vyenye ubora kwa mazoezi.Ukiangalia ubora wa simba ya sasa umejificha zaidi kwenye ubora wa viwanja vyao vya mazoezi .Tangu Simba ikamilishe viwanja vyao ile ndio ilikuwa game changer au au mabadiliko ya kiushindi kwa simba ukipenda utasema hivyo. Kuiga kitu kizuri sio kiburi au dhambi ni uungwana sasa kama Yanga waliona simba walifanya vizuri kumleta Senzo kwa maendeleo ya klabu yao basi wanatakiwa kuiga mfumo mzima wa simba la sivyo Senzo pekee kwa Yanga bila ya mabadiliko ya kiundeshaji itakuwa sawa na mtu aleosha uso ilihali mwili mzima unanuka kwa uchafu wa kutokuoshwa.
ReplyDeleteYanga yatapatapa ishatepeta kwa mnyama, mshafukuza kocha sasa fukuzebi viongozi na GSM wote niwababaishaji
ReplyDelete