August 16, 2020

 


IBRAHIM Ame beki aliyekuwa akikipiga Coastal Union leo Agosti 16 ametambulishwa ndani ya Klabu ya Simba.

Ame amesaini dili la miaka miwili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho Chenye maskani yake Msimbazi.

Anaungana na Pascal Wawa raia wa Ivory Coast mwili jumba kuimarisha safu ya ulinzi.

Pacha wake Bakari Nondo waliyekuwa pamoja naye Coastal Union yupo zake Yanga alikosaini dili la miaka miwili hivyo wamegawana mitaa, Nondo yupo Jangwani na Ame yupo Msimbazi

6 COMMENTS:

  1. Karibu kitasa kipya kamat ya ulinzi

    ReplyDelete
  2. Yupo vizuri anaumbo sahihi kwenye idara yake ya kazi. Mazoezi ya ziada ni muhimu kwani Simba timu yenye ushindani mkubwa wa namba asitishike na majina ya washindani wake ila akikomalie kiwango chake kukieka kunako ubora unaostahiki atafanikiwa kwani tatizo la vijana wetu sio kiwango.Tatizo ni kukosa kujiamini na kujituma kwa malengo.

    ReplyDelete
  3. Bora tusajili tukifungiwa na FIFA watarusaida hawa

    ReplyDelete
  4. Na kweli, ile kesi ya Morisson ukiifuatilia kwa weledi bila ushabiki ni ngumu sana. Argument ya kwamba mkataba upo, inaweza kutugharimu kama rufaa itasikilizwa kwa haki.

    ReplyDelete
  5. Sawa napeleka, we rudisha!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic