August 1, 2020


PIERRE-Emerick Aubameyang, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Arsenal anatajwa kuingia anga za Chelsea ambao leo wanakutana nao kwenye Fainali ya FA jambo lililowashtua mabosi wa timu hiyo.
Aubameyang mwenye miaka 31, raia wa Gabon amekuwa kwenye mvutano mkubwa juu ya kuongeza dili lake jipya ndani ya timu hiyo huku akigoma kuweka wazi kwamba anaweza kuongeza kandarasi ndani ya timu hiyo.
Nyota huyo alimwaga wino ndani ya kikosi cha washika bunduki akitokea Klabu ya Borussia Dortmund kwa thamani ya paundi milioni 56 mwaka 2018 na ametupia zaidi ya mabao 49 ndani ya Ligi Kuu England.
Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard inasaka mshambuliaji kwa sasa ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao na Auba anapewa nafasi ya kuwekwa kwenye rada zake.
Aubameyang ametupia jumla ya mabao 27 kwa msimu huu kwenye mashindano yote pia anatajwa kuingia anga za Barcelona na AC Milan ambao nao wanahitaji saini ya nyota huyo aliye chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.
Mashabiki pia wana mashaka makubwa kuhusu fainali ya leo ambayo inatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:30 Uwanja wa Wembley kwa kuwa wanahitaji matokeo huku tetesi hizo zikiwachanganya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic