AWESU Awesu nyota mpya
ndani ya Klabu ya Azam FC ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili kukitumikia
kikosi hicho amesema kuwa ilikuwa ni ndoto yake kurejea kuitumia timu hiyo.
Kiungo huyo alikuwa anatajwa kuingia rada za Yanga ambao walipishana naye kidogo kabla ya kumalizana na Zawad Mauya ambaye amesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga hivyo malengo yake ya kutaka kureea kwenye klabu yake ya zamani ni sababu kwake kuipotezea Yanga.
Kiungo huyo ambaye
alikuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar na kutupia jumla ya mabao saba kwenye
mashindano yote aliwahi kuwa kwenye kituo cha Azam Academy kwa miaka miwili
2014-15. Kisha akijiunga na Madini ya Arusha,Mwadui FC, Singida United na Kagera Sugar ni timu alizozitumikia kabla
ya kurejea Azam FC
Awesu amesema
kuwa:”Ilikuwa ndoto yangu kurejea ndani ya Azam tangu nilipoondoka niliweka nia
ya kurudi hapa tena ndani ya moyo wangu, Azam ni moja ya klabu kubwa na bora
hivyo ingekuwa ngumu kwangu kugoma kusaini.”
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' amesema kuwa nyota huyo ni
pendekezo la kocha Arstica Cioaba ambaye anahitaji kuboresha kikosi chake kwa
msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment