August 15, 2020


PAPY Tshishimbi, nahodha wa zamani wa Yanga amesema kuwa hana tatizo ikiwa Simba watamfuata ili asaini dili jipya ndani ya klabu hiyo.

Tshishimbi kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na mabosi zake wa zamani, Yanga baada ya mkataba wake kuisha na hakuongezewa mkataba mwingine.

Habari zinaeleza kuwa Simba inahitaji kuinasa saini ya Tshishimbi kutokana na madai ya usumbufu na utovu wa nidhamu wa mara kwa mara kutoka kwa kiungo mkongwe wa timu hiyo, Jonas Mkude, hivyo Papy analetwa kwa lengo la kumpa changamoto.

 

Kingine ni kwamba wameona hakuna haja ya kumleta mchezaji mwingine kutoka nje na Tanzania, ambaye atakuja kuanza upya, hivyo Papy amepewa nafasi kubwa kwa kuwa ni mchezaji huru, lakini pia ameshaijua ligi ya Bongo na anayafahamu vema mazingira ya soka.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba, uongozi wa timu hiyo utakamilisha mazungumzo ya kumsajili kiungo huyo wakati wowote huku wakiwa wamepanga kumpa mkataba wa miaka miwili.

 

“Suala la mazungumzo na Tshishimbi yapo na yanakwenda vizuri kwa sababu uongozi umedhamiria kumleta Simba na ukiangalia yule ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.

 

“Mkakati uliopo ni kumpa mkataba wa miaka miwili na tayari mkataba upo, tayari umeshaandaliwa, ndiyo maana nakwambia haziwezi zikapita siku mbili atakuwa ameshatambulishwa na kuna mambo mengi ya kiufundi yameangaliwa ili timu iweze kupata faida na siyo jambo ambalo watu wamelikurupukia,” kilisema chanzo hicho.


 Tshishimbi amesema:"Naweza kwenda popote pale ambapo nitatakiwa kwenda kucheza kwani mimi ni mchezaji na nipo huru ukizungumzia soka ndiyo kazi yangu sina tatizo katika kucheza.


"Mpaka sasa nina ofa nyingi mkononi hivyo ikikamilika itajulikana wapi nitakuwa kwa ajili ya msimu ujao."




5 COMMENTS:

  1. Msajilini tunajua pesa nyingine alichukua kabla ya nusu fainali ya FA

    ReplyDelete
  2. HAKUNA LOLOTE TUNAJUA WEWE NI MKIA DAMU UNAMPANDISHA TU HADHI HUYO SHISHIBABY MSAJIRINI TU HATUNA MAWAZO NAE KABISAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😆😆😆 Povu Hilo! inauma.

      Delete
  3. Sioni umuhimu wa Tshishimbi pale Simba.Sajilini wachezaji wa maana toka nje kama tunahitaji kupiga hatua za mafanikio.Vinginevyo Kwa usajili wa aina hii basi ni ndoto za alinacha kufikia hatua ya kuingia tena nusu fainali za klabu bingwa Africa.

    ReplyDelete
  4. N Bora tshishibi akacheze na mkude kuliko fraga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic