August 12, 2020


 MWENYEKITI  wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala amesema watatenda haki katika suala la Bernard Morrison dhidi ya Yanga.

 
Mwanjala amesema kuwa kikubwa ambacho wanakizingatia ni haki kwa timu zote mbili pamoja na mchezaji mwenyewe.

Jana, Agosti 11 Mwanjala alisema kuwa sababu kubwa iliyochelewesha maamuzi ya kesi hiyo ni nyaraka moja kukosekana kwa upande wa Yanga na mchezaji mwenyewe Morrison.

Pia alisema kuwa kwa namna mwenendo wa kesi unavyokwenda mambo ni mwendo wa usawa kwa kila timu hivyo ni muhimu kwa wadau kuwa na subira.

Leo Agosti 12 kamati inatarajia kutoa majibu kuhusu maamuzi ya kesi ya Morrison ambaye yeye anasema kuwa ana mkataba wa miezi sita huku Yanga wakisema kuwa ana mkataba wa miaka miwili ambao aliongeza.

Pia alitangazwa kuwa mchezaji wa Simba, Agosti 8 hivyo timu zote mbili zinahusika kwenye kesi hiyo iliyoshika hisia za wadau wengi.

2 COMMENTS:

  1. Hamna kiyu hapo ni ubabaishaji tu mnajifanya muonekano wema mbele ya jamii lakini ni uwongo mtupu ushahidi gani mnao utaka kwani huyo Morison alijieleza mwenyewe kwamba yeye ni Mchezaji wa Yanga ila Simba wanamfuata kumshawishi na kumpa hongo ya $10,000 akasaini Simba kila mtu kasikia hilo sasa iweje leo mambo yamegeuka ghafla na pia aliomba kimaandishi kufuta mkataba wake Yanga kwa madai kapata timu nje ya Nchi na ushahidi pia upo sasa leo iweje mpoteze muda au kuna posho kubwa kwenye hivyo vikao vyenu?

    ReplyDelete
  2. Wa Tz wanamichezo tunadhihirisha unyumbu wetu kupitia sakata hili.........

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic