August 12, 2020

 KIPA namba moja ndani ya kikosi cha Biashara United, Daniel Mgore amesema kuwa kikubwa kinachombeba ndani ya uwanja ni kujiamini na kufanya kazi kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ndani ya kikosi.

Msimu wa 2019/20, Mgore alikuwa ni miongoni mwa makipa waliokuwa wanawania tuzo ya kipa bora ambapo alikuwa akipambana na Aishi Manula wa Simba ambaye alitwaa tuzo hiyo na Nurdin Barola wa Namungo FC.

Mgore amesema kuwa haikuwa rahisi kwake kufika hapo kwani ushindani ulikuwa mkubwa na timu nyingi alizokuwa akikutana nazo zilikuwa zipo vizuri kwa ajili ya kusaka ushindi ndani ya uwanja.

"Haikuwa kazi nyepesi kwangu kufika hapa ila kikubwa ni ushirikiano kutoka kwa wenzangu pamoja na kila mmoja kutimiza majuku yake kwa ukaribu.

"Nina kila sababu za kuwashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi mpaka hapa tulipo sio sehemu mbaya," amesema.


Biashara United imemaliza msimu wa 2019/20 ikiwa nafasi ya 9 na ina pointi 50, Mgore alikusanya jumla ya clean sheet 17.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic