August 1, 2020


NYOTA raia wa Ghana, Bernard Morrison ameingia katika sekeseke jingine baada ya kukamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Morrison alishikiliwa na Polisi ambao waliisimamisha gari aliyokuwa amekodi ya Uber na kumuambia wamesikia harufu ya bangi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, walieleza Morrison akiwa na dereva wa Uber aliwaruhusu askari hao kuanza kupekua kama kweli wameona au wataona bangi, lakini haikuwa hivyo.

"Baadaye wakasema kwamba wanataka simu ya Morrison, jamaa akagoma kuitoa na kucharuka sana akisema hawezi kuwapa na wako tayari wampeleka Polisi.

"Basi ukaibuka mzozo na dereva wa Uber akaanza kuwaamua akiwasisitiza kwamba kama wamehisi kuna bangi kwenye gari wakague kwa kuwa yeye havuti “jani” na wala mteja wake hakufanya hivyo.

Basi wale askari wasisitiza walitaka simu ya Morrison, baadaye wakawachukua wakisema wanawapeleka Kituo cha Oysterbay huku Morrison akisema watu wa Yanga ndiyo wanamfanyia vile,” kilieleza chanzo.

Watu wetu walifika katika Kituo cha Oysterbay na kuelezwa na mmoja wa askari kwamba suala hilo halikuwa kubwa kiasi cha kufikia kuonekana ni kesi.

Morrison amesema.“Nilikuwa njiani nakwenda benki ndiyo wakatokea na kusema vile.Utajiuliza, gari ambayo vioo vimefungwa hata kama kuna harufu ya kitu wewe nje utajuaje!

“Lakini mwisho walituachia na tukaelewana kwa kuwa waliona nilichosema kilikuwa na ukweli na wao walikuwa kazini,” alisema.

Alipoulizwa kweli alihisi ni watu wa Yanga, akasema: “Unajua niko ugenini, ni kweli kabisa ni rahisi kuhisi hivyo hata kama ungekuwa wewe lakini nafikiri yamepita na mimi ninaangalia mambo yangu.”

Kiungo huyo mwenye kasi ameingia kwenye mgogoro mkubwa na Klabu ya Yanga baada ya kusema hana mkataba wa miaka miwili kama inavyoelezwa na uongozi wa klabu hiyo. Morrison amekuwa akisisitiza mkataba wake ni miezi sita na umeisha Julai 14, 2020 na sasa yeye ni mchezaji huru, jambo ambalo Yanga wameendelea kulipinga na kusisitiza, ni mali yao.

Kumekuwa na taarifa kwamba anatakiwa na klabu ya Kuwait na nyingine ya Afrika Kusini lakini taarifa nyingine zinaeleza amekuwa akinusanusa mitaa ya Msimbazi ambao wanataka aongeze nguvu katika msimu ujao huku ikielezwa tayari wameshamvalisha uzi huo mwekundu. Wao Simba, wameendelea kuwa kimya katika hilo.

4 COMMENTS:

  1. Hapakuwa na haja hiyo, police wasijiingize kwenye mambo yasiyo na tija.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walikuwa wanataka wapekue simu yake ili iweje manyani fc ni shida tupu

      Delete
    2. We msenge ujaacha kupakuliwa huko nyuma?

      Delete
  2. Kweli nyie ni mikundu acheni watu wafanye kazi zao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic