UONGOZI wa Klabu ya Simba umefunguka kuwa safari hii hawatarajii kuwa na Tuzo za Mo kama walivyofanya misimu miwili iliyopita kutokana na muda kutokuwa rafiki kwao.
Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ imekuwa na utaratibu wa kuwapa tuzo wachezaji wa kikosi hicho pamoja na viongozi wa benchi la ufundi katika misimu miwili mfululizo iliyopita kutokana na kutambua mchango wao.
Katika msimu uliopita wachezaji kadhaa waliweza kukabidhiwa tuzo akiwemo mshambuliaji bora, Meddie Kagere.
Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe alisema: “Safari hii hatutakuwa na Tuzo za Mo kutokana na kipindi kile cha Corona ligi ilisimama miezi mitatu, baadhi ya wachezaji walibaki hapahapa hawakuondoka, hivyo kwa sasa wanahitaji kupata mapumziko mafupi kabla ya kuanza msimu mpya.
“Wachezaji wa kimataifa wanatakiwa wapate mapumziko na kipindi cha maandalizi ya msimu mpya, pia tunahitaji kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.”
Chanzo: Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment