KIUNGO wa Simba, Luis Miquissone leo Agosti 2,2020 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.
Simba imseshinda mbele ya Namungo leo kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Luis amehusika kwenye mabao yote mawili ya Simba akifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya bao kwa John Bocco.
Nyota huyo amesema:"Ninafurahi kuona timu inapata matokeo na kupata ushindi jambo ambalo ninalifurahia.
"Mimi ni kiungo ila naona nabadilika na kuwa mshambuliaji ninafunga na kutengeneza nafasi kwani ni timu na kazi tunafanya kwa kushirikiana hilo ni jambo jema na furaha kwetu."
Hili linakuwa ni taji la pili kwa Luis akiwa na Simba baada ya kuanza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na leo la Shirikisho.
Luis amefunga jumla ya mabao mawili ndani ya Kombe la Shirikisho, bao lake la kwanza aliwatungua Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-1 na kuwapa tiketi ya kushiriki fainali ambayo wameshinda leo.
Simba wako vizuri sana sasa naamini maneno ya Mfalme Manara back to back 10 yrs
ReplyDeleteBado 07yrs
ReplyDelete