August 19, 2020


HASSAN Dilunga na Said Ndemla, viungo wa Klabu ya Simba bado wataendelea kukipiga ndani ya kikosi hicho cha Mabingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo baada ya kuongezewa mikataba ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka miwili.

Nyota hao wote wawili ndani ya msimu wa 2019/20 wamehusika kwenye jumla ya mabao 12 kati ya 78 ambayo yamefungwa na Simba iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo ikiwa na pointi 88.

Dilunga alitupia mabao 7 na pasi tatu za mabao huku Ndemla akifunga bao moja na kutengeneza pasi moja ya bao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Agosti 30,itakuwa na kazi ya kumenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii huku kwenye Ligi itaanza kumenyana na Ihefu FC, Septemba 6, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Chanzo:Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic