PSG imekuwa timu ya kwanza kutoka Ufaransa kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Klabu ya Leipzing huku mchezaji wa zamani wa Manchester United, Angel di Maria akiwa shujaa wa mchezo huo.
Di Maria alikuwa ni moto wa kuotea mabali, alitoa pasi ya kwanza ya bao kwa mtupiaji Marquinhos dakika ya 13 naye pia alifunga bao la pili dakika ya 41 huku lile la mwisho likipachikwa dakika ya 52 na Juan Bernat dakika ya 52.
Nyota yake ilingarishwa na Klylian Mbappe pamoja na Neymar Jr ambao wamekuwa ni wachezaji muhimu kwenye kikosi hicho ambacho kilikuwa hakipewi nafasi ya kufanya makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwanzoni.
Mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Agosti 23 na itasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Bayern Munich ambao walitinga hatua ya nusu fainali kwa kuinyoosha kwa mabao 8-2 Barcelona huku Lyon wao wakiwanyoosha Manchester Unted mabao 2-1.
Ache uongo nyie muwe mnafatilia vzr habar zenu man United na Lyon wamacheza Lin Kwan bingwa?
ReplyDelete