August 21, 2020

 


MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ndani ya msimu wa 2020/21 mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya JKT Tanzania,utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.

Maxime alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Yanga ili kuvaa mikoba ya Luc Eymael ambaye alifutwa kazi Julai 27 bado atazidi kuwa ndani ya kikosi hicho baada ya uongozi wa timu hiyo kusema kuwa hauzwi.

Akimalizana na JKT Tanzania, Septemba 7 atakutana na Gwambina FC, Septemba 11 atakuwa ugenini kisha kazi yake nyingine itakuwa mbele ya Yanga, Septemba 19 Uwanja wa Kaitaba.

Atamaliza mwezi Septemba akiwa Kaitaba kwa kumenyana na  Klabu ya KCM, Septemba 25.

Tayari kwa sasa Kagera Sugar wameanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine watakayoshiriki ndani ya msimu wa 2020/21.

2 COMMENTS:

  1. ATAFUNGWA 4 -0 NA YANGA MWAKA HUU MWEZI SEPTEMBA PALE UWANJA WA KAITABA NA MSIMU UNAOKUJA KAGERA SUGAR INAWEZA KUSHUKA DARAJA.YANGA HATACHUKUA UBINGWA UTACHUKULIWA NA SIMBA ILA YANGA ATASHIKA NAFASI YA PILI KWA TOFAUTI NDOGO YA POINT NA BINGWA, YANGA ATASHINDA KOMBE LA FA KWA KUMFUNGA AZAM FC AMBAE ATAKUWA AMEMTOA SIMBA KWA PENATI. YANGA ATAMTOA NAMUNGO KTK NUSU FAINALI YA FA NA FAINALI ATAKUTANA NA AZAM FC. WEKA KUMBUKUMBU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😆😆ndumba hizo, mpira nisayansi acha ndumba ww

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic