NAMUNGO FC inayonolewa na Kocha Mkuu Hitimana Thiery ni miongoni mwa timu ambazo zimeonyesha ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara hata kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho.
Licha ya wachezaji wake wengi muhimu kuwa wagonjwa bado aliweza kuonyesha ushindani mbele ya Simba kwenye mchezo wa fainali uliochezwa jana, Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela.
Thiery hakuwa na chaguo baada ya mshambuliaji wake namba moja, Relliants Lusajo mwenye mabao 12 kuwa mgonjwa aliamua kujitoa muhanga kwa kumtumia Edward Manyama.
Manyama ambaye alitupia bao kwa upande wa Namungo FC naye pia hakuwa fiti asilimia mia kwani naye pia alikuwa ametoka kuugua hivi karibuni.
Thiery amesema:"Nilikuwa na wachezaji wengi wagonjwa ila naona wamepambana na kupata kile ambacho tumepata, bado tuna safari nyingine lazima tuzidi kujipanga.
"Kucheza na bingwa sio jambo jepesi kwani kila mchezaji wa Simba ni bora na wameonyesha utofauti wao."
Nurdin Barola kipa wa Namungo FC alikuwa ni nyota wa mchezo kwa kuwa alifanya save moja matata baada ya nahodha wa Simba, John Bocco kuudokoa mpira kidogo kwa juu akiwa eneo sahihi la mpinzani ukakutana na mikono ya Barola aliyeweka lango salama.
Simba ilishinda kwa mabao 2-1 baada ya dakika 90 na kusepa na taji pamoja na hundi ya milioni 50.
Bao pekee la Namungo lilipachikwa na Edward Manyama akiunganisha pasi ya kona ya Abeid Athuman huku yale ya Simba yakifungwa na Luis Miqussone na John Bocco.

Tuombe ushindi uendelee ndani na nje Bila ya yeyote kuumizwa kwa hayo kwani sifa zinanyanyua sio kwa Simba tu Bali kikubwa ni kwa nchi yetu
ReplyDeleteInaonyesha mwandishi wa hii mskala hakupenda simba ishinde kabisa kwani uwanjani kondeboy kapewa nyota wa mchezo yeye anasema kipa wa Namungo halafu pia anajua mpaka afya za wachezaji utafikiri yeye ni daktari wa timu
ReplyDeleteHuyu Yanga. Hujaona hata usajili wa Yanga anaandika breaking news, lakini wengine wakisajili hasemi hivyoo, huyu timu uto
DeleteAisee, kumbe aliyepewa sh. laki tano za zawadi ya mchezaji bora wa mechi ni kipa wa Namungo? Mimi nilidhani eti yule alikuwa ni Luis Miquisonne
ReplyDeleteBila ya kusahau pitch ya ule uwanja simba kupata matokeo walioyapata kwa kweli wanastahili pongezi. Kwenye ile mechi mchezaji wangu bora ni shomari kapombe. Simba ili kufanya vizuri kimataifa lazima watafute fowadi wa kuzitumia kwa manufaa ya kutosha cross za shomari kapombe. Au wawatrain washambuliaji wake jinsi ya kuitumia mipira ya kapombe kufunga mabao ya haraka haraka. Kapombe ni big asset ndani ya Simba ila mbele pale bado hakujawa na mtu sahihi wa kucheza nae yaani wa kuunganisha ule uwezo wake mkubwa wa kupiga cross na kuinufaisha Simba katika kutengeneza magoli. Cross zake nyingi ambazo ni magoli ya wazi hupotea hivi hivi tu.
ReplyDeleteMwandishi anaandika kwa ushabiki haswa.Anajulikäna kwa unazi. Maendeleo ya Simba yanamkera. Hata zile makala za muuaji wa Simba sasa zimepotea baada ya 4 G.
ReplyDeleteMwandishi alikuwa na nytta wake wa mchezo. Sio yule aliyetangazwa na kupewa laki 5.Unazi ugonjwa mbaya hasa kwa Mwandishi wa blogu hii.
ReplyDelete