August 13, 2020

 


UONGOZI wa Namungo FC upo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humud na beki wa kushoto wa timu hiyo Issa Rashid maarufu kama Baba Ubaya.


Namungo FC tayari imeshaikosa huduma ya mshambuliaji wake, Reliants Lusajo ambaye alitupia mabao 12 ndani ya ligi na msimu wa 2018/19 kwenye Ligi Daraja la Kwanza alitupia mabao 15.


Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu amesema kuwa hesabu zao kwa Lusajo zimekwisha wanatazama namna ya kuboresha kikosi hicho kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu.


"Ipo wazi hatutakuwa na Lusajo msimu ujao lakini lazima tujipange kupata wachezaji makini na wenye uwezo ndani ya timu yetu hivyo tayari tumeshaanza kufanya mazungumzo na wachezaji ambao ni pendekezo la mwalimu.

"Humud na Kibaya ni miongoni mwa wachezaji ambao tunawahitaji hivyo mambo yakikamilika kwa utaratibu ulivyo basi tutajua tunafanyaje na kila kitu kitakuwa wazi,".


Chanzo:Spoti Xtra

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic