August 13, 2020

 


UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa unaachana na nyota wao tisa baada ya mikataba yao kuisha kwa msimu wa 2019/20.

Katibu wa timu hiyo, Ally Masoud amesema kuwa wamefanya hivyo kulingana na ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Meck Maxime.


"Wachezaji wapatao tisa mikataba yao imeisha na kuelekea msimu ujao hatutakuwa nao ndani ya kikosi tunawashukuru kwa huduma yao.


"Wachezaji ambao tumeachana nao ni :-Juma Nyosso, Ally Shomary, Juma Shemvuni,Majidi Bakari,Frank Ikobela,Evarist Mujwahuki,Kelvin Sabato na Geofrey Mwashiuya,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic