August 18, 2020

 


SAID Ndemla, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, leo Agosti 18 ameongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kutumika ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi.

Msimu wa 2019/20, Ndemla amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza akijenga urafiki mkubwa na benchi huku nafasi yake ya ukabaji ikiwa mikononi mwa Jonas Mkude.

Kwenye mabao 78 ambayo yamefungwa na Simba amehusika kwenye mabao mawili ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara.

1 COMMENTS:

  1. Safi ni miongoni mwa wachezaji watiifu sana kuwahi kutokea simba ila apambane ningefurahi siku moja kumuona said Ndemla pale simba akiwa kapteni wa kutegemewa ndani ya kikosi cha Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic