RASMI leo Agosti 14, Charlse Ilanfya ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven.
Ilanfya alikuwa anakipiga ndani ya KMC ambapo aliibukia huko msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Mwadui FC.
Nyota huyo ni chaguo la Sven ambaye aliwaambia viongozi wa Simba wampe mkataba nyota huyo alipomuoana akiwa na jezi ya KMC.
Ndani ya ligi alipokuwa KMC, Ilanfya alitupia mabao 6 kati ya 35 yaliyofungwa na timu hiyo iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya 13.
0 COMMENTS:
Post a Comment