August 5, 2020



NYOTA watano wa kikosi cha Ruvu Shooting wameachwa jumlajumla ndani ya kikosi hicho hivyo msimu wa 2020/21 hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho. 

Benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga lilitoa ushauri huo huku wakiwa na mpango wa kusajili wachezaji wengine wapya watano.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema:-"Leo Agosti 5 uongozi umekaa kikao na kuanza utekelezaji kwa ajli ya msimu ujao ili kuboresha kikosi chetu.

"Wachezaji walioachwa ni pamoja na Zair Rajabu, Jamal Mnyate, Salum Makota, Edward Christopher na Adam Faraja,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic