August 5, 2020



TIMU ya Simba Queens leo Agosti 5 imeibuka na ushindi wa mabao 5 -0 mbele ya  Baobab Queens kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mabao ya Simba yalifungwa na Mwanahamisi Omary aliyetupia mawili,Opah Clement alitupia bao moja, sawa na Dotto Evarist  huku kipa Zubeda Mgunda akitupia bao moja kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi wa leo unaifanya Simba Queens kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Wanawake kwa kuwa wamefikisha jumla ya pointi 53 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote kwa sasa ndani ya ligi hiyo.

Imebakiwa na mechi mbili za kucheza ambazo ni dhidi ya Alliance Girls  na TSC Queens yote hiyo itakuwa kanda ya ziwa Ushindi huo unaifanya kuivua JKT Queens ubingwa jumlajumla kwa kuwa msimu uliopita ilitwaa taji hilo.

1 COMMENTS:

  1. Hongereni dada zetu kwakunyakua ubingwa mapema Kama kaka zenu, brand ya Simba inazidi kupaa. Sasa bado ubingwa wa Afrika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic