August 20, 2020

 

BAYERN Munich usiku wa kuamkia leo imeshinda kwa mabao 3-0 mbele ya Lyon kwenye mchezo wa nusu fainali hatua ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 


Mabao ya Munich mawili yalifungwa  na Gnabry dadakika ya 18 na 33 na lile la tatu lilifungwa na mshambuliaji wao machachari Lewandowski dakika ya 88.


Sasa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayotarajiwa kuchezwa Agosti 23 itakuwa ni dhidi ya PSG. 


Uzuri ni kwamba timu zote zinatinga fainali zikiwa zimetoka kupata matokeo yanayofanana kwenye hatua ya nusu fainali. 


PSG nayo ilitinga hatua ya fainali kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Leipzig hivyo mwenye kisu kikali ndiye atasepa na taji hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic