UONGOZI wa Simba umesema kuwa kiungo wao mshambuliaji Ibrahim Ajibu hakuwa na nafasi ndani ya kikosi cha kwanza kwa kuwa falsafa ya timu hiyo ni lazima kuwe na ushindani wa namba.
Ajibu ambaye ameibukia Simba msimu wa 2019/20 ametwaa mataji matatu ikiwa ni pamoja na lile la ngao ya jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho huku akitumia muda mwingi kukaa benchi.
Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mechi tatu za mwisho ikiwa ni mbili za ligi ile ya Coastal Union na ya mwisho ya Polisi Tanzania pamoja na mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC, uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna utofauti mkubwa wa Simba na Yanga alipokuwa hasa linapokuja suala la ushindani wa namba.
"Dunia nzima inajua, hata mashabiki wanajua kwamba Ajibu alipokuwa Yanga kule alikuwa mfalme kwa kuwa alikuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza ila alipokuja Simba mambo yamekuwa tofauti namba lazima ugombanie.
"Kila kiungo anajua hebu angalia kuna Francis Kahata, yupo Luis Miqussone, Clatous Chama lakini hata hao wanaanzia benchi muda mwingine hivyo ni sera ya Simba kila namba iwe na watu wakaliwakali," amesema.
Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa nyota ambao watatolewa kwa mkopo ni pamoja na Ajibu ambaye anaweza kuibukia Namungo FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment