August 1, 2020


ZIMBEBAKI saa chache kabla ya fainali ya Kombe la Shirikisho, kati ya Simba na Namungo kupigwa kesho, Agosti 2, Uwanja wa Nelseon Mandela, Sumbawanga.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa licha ya maandalizi waliyokuwa nayo kwa siku kadhaa lakini anaona Uwanja wa Nelson Mandela unaweza kumuharibia.

Kocha huyo ameongeza kuwa, licha ya yote hayo lakini bado hesabu zake zote ni kuhakikisha kwamba ubingwa wa kombe hilo anautia mkononi.

Sven raia wa Ubelgiji amesema kuwa uwanja huo unaweza kuwa kikwazo kwao kutokana na kutokuwa sawa kwa asilimia 100 lakini hawana namna zaidi ya kupambana na wapinzani wao.

“Hii ni mechi muhimu kwetu na tumekuwa na maandalizi nayo kwa kipindi kirefu, tukianzia na zile mechi mbili za mwisho za ligi kabla ya kwenda Mbeya.

 “Itakuwa ngumu na tunatakiwa kujiweka sawa zaidi kuliko wapinzani kwa sababu ya wapinzani wetu walivyo lakini pia aina ya uwanja ambao tutauchezea.

“Uwanja siyo mzuri sana lakini hakuna namna zaidi ya kupambana kwa sababu lengo letu tunalolitaka ni kuona tunashinda ubingwa huu kama ambavyo tumekuwa tukitamani kuona tunafanikisha hilo,” alimaliza Sven.

Simba ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga huku Namungo FC ikishinda kwa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars.

5 COMMENTS:

  1. Hao waandaaji ovyo kabisa. Kwanini walipeleka fainali huko huku wakijua uwanja ni mbovu? Kulikuwa na ulazima wowote wa fainali kuchezwa huko?

    ReplyDelete
  2. Walipewa muda mrefu wa kuandaa Uwanja lakini hawajafanya lolote la maana. Ni kashfa kubwa kwa TFF na waandaji wa Uwanja.

    ReplyDelete
  3. Wazo la kupeleka ASFA mikoa mbali mvali ni zuri lakini dosari ni VIWANJA. Kambumbu bila viwanja vizuri hainogi.Maendeleo ya mpira kwenye Nchi yeyote ni miundombinu hasa VIWANJA vizuti. Bila VIWANJA vizuri hatutaendeleza mpira wetu.

    ReplyDelete
  4. hats kams lengo ni kupeleka mikoani wapeleke mechi za mchujo sii nudu fainal au fsinsl

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic