August 14, 2020

 


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa unasubiria nakala ya hukumu kutoka kwenye Kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya maamuzi yaliyotolewa kwa kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison kabla ya kwenda ngazi ya juu zaidi.

 

Juzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala alimtangaza Morrison kushinda kesi hiyo kuhusu sakata la kudaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga kuwa na kasoro kisha baadaye kumpa nafasi ya kuchagua timu ya kuichezea kwa ajili ya msimu ujao.


Wakati Mghana huyo akishinda kesi hiyo, ameamuliwa kurejesha fedha za Yanga alizozichukua ambazo ni dola 25,000 (zaidi ya Sh 58Mil) huku akipelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kutokana na kosa la kusaini mkataba Simba akiwa kwenye kesi hiyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kamwe hawatabadili maamuzi waliyoyatoa ya kwenda kushtaki kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Kimichezo ya Kimataifa (CAS) pamoja na Fifa.


Mwakalebela amesema kuwa mara baada ya kupata nakala ya hukumu, haraka wataanza taratibu za kwenda CAS kwa ajili ya kupinga maamuzi hayo yaliyotolewa na TFF.


Aliongeza kuwa mapungufu ambayo yametolewa na kamati hiyo ya TFF hayapo katika mkataba wao, labda kama wanayo mengine mapya ambayo hawayajui.

 

“Tunasubiri nakala ya hukumu, ili tukate rufaa CAS, kwani bila nakala hiyo CAS hawatatupokea, hivyo ili tupokewe ni lazima tuipate nakala hiyo ya hukumu ambayo ninaamini ndani ya siku hizi mbili tutaipata.

 

“Kama uongozi tumeshangaa na mapungufu wanayoyataja kamati hiyo ambayo hayapo katika mkataba labda kama wanao mwingine. Mkataba tulioutoa mbele ya kamati hauna hayo mapungufu,” alisema Mwakalebela.


Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa baada ya hukumu hiyo jana alisikika akisema: “Katika mkataba ni jambo la kawaida kutokea utofauti wa tarehe, hivyo tarehe haiwezi kufanya mkataba kuwa batili, Je aliwezaje kupokea pesa bila kuwa na mkataba!”


Katika hatua nyingine Mwekezaji wa Simba, Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’, jana kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii alimkaribisha kiungo huyo na kumpa onyo kwa kumwambia:“Karibu Simba, Bernard Morrison. Tunaamini utakuja kuwa sehemu ya kuendeleza na kukuza misingi tuliyojiwekea ya nidhamu, kujituma na kujali maslahi ya klabu kwa jumla.”

10 COMMENTS:

  1. Kila la kheri, ila kumbukeni aliyedaiwa kumsainisha ni gsm na hatambuliki ktk uongozi wa yanga

    ReplyDelete
  2. Viongozi wa Yanga hebu achaneni na huyo MZEE MEKO.....kuendelea kumng'ang'ania ni kuwavunjia heshima wachezaji wengine hasa wachezaji wazawa kwa kuwaonesha kuwa hawana uwezo kuliko huyo mtu mmoja,mnatumia nguvu nyingi za akili kwa ajili ya mchezaji mmoja kisa tu mbwembwe zake za uwanjani na kuacha ku deal na mambo ya msingi.Kukubali yaishe ni ukomavu wa uongozi kuliko kupoteza muda kwa ajili ya mchezaji mmoja.

    ReplyDelete
  3. hv yanga wakimpata morson atacheza kweli au atalipwa mshahara wa bure?

    ReplyDelete
  4. Huko cas yatafumuka mengine ikiwemo kusajiliwa na kucheza mechi bila mkataba wanasheria hizo kesi hawaendeshi bure tff waliamua hivyo kufunika mambo yapite jiulize kwanini pamoja na kupeleka saini ya Morison polisi hawakusema kama saini imesajili au la

    ReplyDelete
  5. The Court of Arbitration for sport yaani CAS sio kitu cha kusema tu kirahisi tutakimbilia huko.Kama Yanga wanapesa hazina kazi basi waache waupamde mkemge waende huko CAS.Wajiandae tu Yanga na gharama ya kesi, pesa ambayo wangeweza kuitumia kusaini mchezaji yeyote Africa wanaemtaka zaidi ya Morrisoni,akili ni kufikiri kabla ya kufanya jambo bila ya kukurupuka. Kwanza shauri dogo tu kusikilizwa kule CAS linaanza kusikilizwa baada ya miezi mitatu.Na si kwamba shauri la Yanga huko CAS litakuwa la Yanga pekee yake hapana,Morrison atakuwa huko na mwanasheria wake kama atakuwa nae,TFF na wanasheria wao pia watakuwa huko,Simba nao na mwanasheria wao pia watakuwa huko,FIFA nao na wanasheria wao pia watakuwa hapo ambapo ndio nyumbani kwao. Kwa hivyo ni kuelimishana kidogo tu kuhusiana na hii CAS yenye makao makuu yake Lausanne Uswiss sio sehemu ya wanafiki kwani wanatumia mpaka X-ray kutafiti vitu kama signatures yaani saini husika kama ni feki au la nakadhalika.

    ReplyDelete
  6. haya waende na mkataba ambao kipende cha saini kimechanwa..documents zilizopelekwa TFF ndio hizo hizo zitapelekwa CAF

    ReplyDelete
  7. Jamaa wanajaribu kuitisha TFF kwani wanajuwa vema kuwa saini haikuwa ya Morrison na mkataba ilikuwa kipande tu na kwa hayo hawajakanusha isipokuwa kufanya Hayo ni dharba walioipata inawatia kizunguzungu

    ReplyDelete
  8. Wanangoja nakara ya hukumu Kijana tulianZishe ,mimba inabebwa na mwanamke siyo mwanaumme

    ReplyDelete
  9. Tunataka kutoa fundisho kwa wale wanajifanya tff yao

    ReplyDelete
  10. Ala leo mnasema GSM hatambuliki. Ama hii kali je itakuwaaje akisema kama hatambuliki atatuwa mzigo. Lakini Hawa wanakijuwa wanachokisema au kulifanya au ndio mnataka ayabebe yeye na nyie mumruke kimanga? Tutaona mengi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic