September 26, 2020


 AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu Aristica Cioaba leo Septemba 26 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.


Bao pekee la ushindi limepachikwa kimiani na nyota wao mpya Prince Dube dakika 90 kwa kichwa ndani ya 18 akimalizia krosi iliyochongwa na Idd Naldo akiwa nje ya 18.


Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walijitokeza kuutazama.

Azam FC inaweka rekodi ya kushinda mechi zake mbili mfululizo ikiwa ugenini baada ya kuanza kushinda mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokone kwa bao 1-0 kiaha leo mbele ya Prisons kwa bao 1-0.

Jumla inakuwa imeshinda jumla ya mechi nne ambapo ikiwa Uwanja wa Azam Complex ilishinda mechi mbili ilikuwa ni mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa haikuwa kazi rahisi ila mwisho wa siku wamesepa na pointi tatu muhimu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic