UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauwezi kuzungumzia ishu ya kuitaka saini ya nyota namba moja ndani ya Simba, Clatous Chama.
Chama amekuwa akitajwa kuondoka ndani ya Simba huku habari zikieleza kuwa miongoni mwa timu ambazo zinaitazama saini yake kwa ukaribu ni pamoja na Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krompotic.
Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawezi kuzungumzia suala la Chama kwa kuwa hajui chochote kuhusu suala hilo.
“Kuhusu Chama kiukweli siwezi kulizungumzia kwa sasa nisije nikawa muongo, sijui chochote kuhusu Chama ila ninachojua mimi tuna kikosi kizuri ambacho kinashindana ndani ya ligi na nina imani tutafanya vizuri,” amesema Mwakalebela.
Chama mkataba wake ndani ya Simba unameguka Julai 21 ambapo akiwa ndani ya Simba msimu uliopita aliweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora na kiungo bora kwa msimu wa 2019/20.
Manara keshasema hamna uwezo wa kutoa daw wala mishara wake.
ReplyDeleteKwani manala si anafanya kazi anategemea kulipwa hayo ni maneno2 yanga tunauwezo hata wa kumleta hazard kwanini tushindwe chamaz
DeleteYanga tuwe na subira tukamilishe mchakato tuliouanzisha wa mageuzi ili kujua mgawano wa hisa. Kwa sasa GSM si mwekezaji wala mfadhili aliyeidhhinishwa na wenye timu yao ambao ni "wananchI". GSM ni mfadhili mwenye mapenzi na timu
DeleteHii habari haina maana, wewe mwandishi unasema bosi wa yanga azungimzia kuhusu chama, kwenye habari yenyewe umeandika amesema hajui chochote sasa hapo kuna nini kama sio fale news.
ReplyDeleteHatakama wanamtaka hawezi kusema hadharani, kwa watu makini mipango haiwekwi hadharani.
ReplyDeleteYashapita hayo mwandishi zilipe dwa hbr hizo mpaka makam makam mwenyekiti aliomba radhi kwa wanasimba suala la chama na kesi IPO tff. Sasa ww inatuletea zilipendwa ukijua ymutopoko bdo Ni makabwela shiboub,sure boy wanechemka kuwapata ndo wamueze chama thubutuu?
ReplyDeleteOnly time will tell us
ReplyDeleteUtopolo wamemshindwa sure boy
ReplyDelete