September 27, 2020




 OFISA Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ushindi ambao wameupata jana umetokana na juhudi za wachezaji kujituma ndani ya uwanja pamoja na sapoti kubwa za mashabiki kujitokeza kwenye kila mchezo.

Jana Septemba 26, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwaja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thabit amesema kuwa ushindi huo unarejea kwa mashabiki kwa kuwa wamekuwa wakijitokeza kwenye mechi zote bila kuchoka.

"Ushindi ambao tumeupata ni maalumu kwa ajili ya mashabiki na wachezaji wanatambua kwamba ni muhimu kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza kwani malengo ni kuweza kufikia malengo ambayo tunayahitaji," amesema.


Azam FC inaongoza ligi ikiwa imecheza mechi nne mfululizo bila kufungwa na nyavu zake hazijaguswa mpaka sasa ikiwa imefunga mabao manne ndani ya dakika 360.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic