MENEJA wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amesema kama Kocha wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck atampa nafasi mshambuliaji wake huyo basi ataendelea kuwakera wapinzani kwenye ligi ili atetee kiatu chake.
Kagere amefanikiwa kutwaa ufungaji bora misimu miwili mfululizo, 2018/19 alifunga mabao 23 na ule wa 2019/20 akitupia 22.
Hivi karibuni, Gakumba alitoa malalamiko juu ya mchezaji wake huyo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza hali iliyosababisha Sven ampange kwenye mechi dhidi ya Biashara United ambapo alifanikiwa kutupia bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Simba waliupata.
pia jana wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC alianza Kagere na alitupia bao moja.
Gakumba amesema anauamini uwezo wa Kagere kwa asilimia zote na iwapo atapewa nafasi zaidi kama ilivyo misimu iliyopita basi atatwaa kiatu cha dhahabu.
“Nashukuru uongozi wa Simba na mwalimu kwa nafasi aliyompa Kagere kwa kumuamini kwani ameleta furaha kwa Wanyarwanda ambao wamekuwa wakimfuatilia sana ndiyo maana APR ilikuwa ikimnyatia sana na walinifuata baada ya kuona hachezeshwi.
“Kagere ni mchezaji anayeelewa nini cha kufanya anapokuwa uwanjani, nimefurahi kuona amepata nafasi na amethibitisha kuwa bado ni yuleyule na ameonyesha uwezo, lakini naamini bado hajaonyesha kiwango chake, mechi za kimataifa ndio atakera sana.
“Iwapo ataendelea kupewa nafasi ndani ya kikosi cha Simba basi nina uhakika wa kuweza kutetea nafasi yake ya ufungaji bora kwani ni mchezaji mwenye kiwango kizuri hakuna asiyejua,” amesema Gakumba.
WANANCHI LEO TUNA JAMBO LETU PALE JAMHURI. KARIBUNI TUMWONE TK MASTER, MUKOKO TONOMBE, LAMINE MORO NA SONGNE ENJOY FOOTBALL. ACHANA NA MABABU HAO, TIMU INAWASTANI WA MIAKA 33 UMEONA WAPI DUNIANI. TIMU NDOGO KAMA GWAMBINA ZINAHITAJI KUTIWA MOYO NA MAREFA.
ReplyDeleteYote magarasa hayo
Deletemnyama mwendo mdundo wape wapenzi wako raha. maneno mengine ni wivu tu ndio ynawasumbua watu..hasa wakikukumbuka 4G.nyie na wao wapi na wapi!
ReplyDeletemnyama mwendo mdundo. kama kawaida 18 october ni 4G kwa utopolo.
ReplyDeletembona husomike
ReplyDeletemara uko yanga mara simba
ReplyDeleteBora wametusaidia kutuondolea Morrison alikuwa anaharibu mwonekano wa timu
ReplyDeleteHabaro ni kagere, watu wamerukia kuelezea wachezaji wa yanga, kulikoni? Hao unaosema wazee ndio mabingwa, na hao watoto wacha waendelee kujifunza kwanza wakikua watapata ubingwa
ReplyDeleteHabari kweli ni Kagere "Mzee". Unganisha story vizuri. Ni aina tu za uandishi.
Delete