September 23, 2020


 MENEJA Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hapati usumbufu wowote kutoka kwa kiungo mshambuliaji wake mpya Mghana, Bernard Morrison.

 

Mghana huyo akiwa anaichezea Yanga inasemekana alikuwa akiwafanyia vioja na usumbufu uongozi wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Simba kwenye msimu huu.

 

Kati ya vioja na usumbufu ambao aliwahi kufanya akiwa na Yanga ni kuondoka kambini bila ya ruhusa kutoka kwa uongozi wakati timu hiyo ikiwa kwenye hoteli moja Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

Rweyemamu amesema kuwa amefurahishwa na nidhamu kubwa anayoendelea nayo Morrison tangu ajiunge na timu hiyo kwenye msimu huu.


Rweyemamu amesema kiungo wake huyo anaishi vizuri na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi wakati wakiwa kambini.

 

“Morrison mbona yupo freshi hana tatizo na mtu, anaishi vizuri na wachezaji katika maisha ya tofauti nje na ndani ya uwanja, hivyo kwangu najisikia furaha.

 

“Tangu Morrison alipojiunga na Simba hakuwahi kuleta usumbufu wowote zaidi ya kutoa ushirikiano kwa wachezaji wenzake kwa kila jambo linalotokea ndani na nje ya kambi.

 

“Morrison ni mcheshi anayependa kujichanganya na wachezaji wenzake zaidi hajawahi kuleta usumbufu wowote ndani wala nje ya kambi na kwangu ana nidhamu ya hali ya juu,” amesema Rweyemamu.

6 COMMENTS:

  1. Kilichomfanya kuikimbia Yanga ni kutokana na ile zomeazomea ambayo ilikuwa inamuumiza sana na kuwepo Kwake ndani ya Simba Kumempa afuweni na kuona maisha matamu sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekana ni kweli kuzomewa kwa kiasi kikubwa ni jambo lenye changamoto, linaweza likampoteza mtu malengo yake.

      Delete
  2. Tunapongeza sana, hali hiyo tunatarajia aendelee hivyo hivyo kwa manufaa ya Simba Sports Club na mchezo wa Soka Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Subirini maana vimbwanga sio vioja.

    ReplyDelete
  4. Morrison anahita mafanikio hivyo hawezi kukaa na mdebwedo wanaoshindis mihogo na kusainidha watu mikataba feki. Morrison keshokutwa tu utasikia anapaa ulaya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic