YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja wa Kagera Sugar amesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara licha ya ushindani kuwa mkubwa kwa msimu wa 2020/21.
Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Maxime ilishinda mchezo wake wa kwanza mbele ya KMC baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kuambulia ushindi.
Ilianza kwa kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Kaitaba ikalazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC Uwanja wa Gwambina Complex kisha ikapokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga.
Iliitungua KMC bao 1-0 lililopachikwa na Mhilu kwenye mechi yake ya kwanza baada ya kukosekana kwenye mechi tatu za ligi za msimu wa 2020/21.
Nyota huyo amesema:"Ushindani kwa msimu wa 2020/21 ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi kwa namna ambavyo tunajipanga nina amini tuna nafasi kubwa ya kuendelea kuwa imara.
"Kikubwa mashabiki ambao wapo pamoja nasi waendelee kutupa sapoti kwani kwa kufanya hivyo nasi pia tunakuwa na furaha na kushindana bila kuchoka."
Msimu wa 2019/20 Mhilu alikuwa na mwendelezo mzuri wa kutupia kwani alikuwa mzawa mwenye mabao mengi ndani ya tano bora ambapo alitupia mabao 13.
Hivi kwanini yusuph muhilu hakucheza mechi tatu hizo alikuwa majerui au mwenye taarifa atupe jamani
ReplyDelete