September 26, 2020


 MFALME wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba maarufu kama Alikiba, amefunguka mambo mazito yaliyo nyuma ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mediocre‘ ambao mashabiki wengi mitandaoni wamedai kuwa amewaponda wasanii wenzake Diamond na Harmonize, ikiwa ni miezi mitatu tangu alipoachia ‘So Hot’.

 

Akizungumzia ngoma hiyo, Kiba amesema idea ya wimbo huo ilikuja katika mizuka ya studio, ilipigwa ‘beat’ na yeye akaona  ajaribu kurap.

 

“Kila kitu nilichoimba kwenye Mediocre kina make sense, Kila mtu amejibrand na watu wamempokea vile walivyompokea, Sio kila mtu anaweza kuwa King, kuna watu wamejiita marais, kuna watu wamejiita makomando, stick from what you have.

 

“King huwa ni mmoja tu, hata kama akilala watu wanajua King amelala, na hakuna wa kuchukua nafasi yake mpaka afe, siyo kila mtu anaweza kuwa King. Wakati huu kumekuwa na mambo mengi ambayo to me, naona they are so Mediocre.

 

“Kuna watu wanatamani kuwa ma-King wa mafundo, wanafanya vitu vingi, unamkuta amejifunga mara mavitambaa au amevaa madude sehemu, vitu flani vinakaa kaa tu, they wish lakini wanatumia njia nyingi sana ili kuwaaminisha watu kuwa ndo mie ilimradi awe,  kumbe King is here to stay, wanatumia njia nyingi lakini King ni mmoja!,” amesema Kiba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic