KLABU ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini leo Septemba 26 imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.
mchezo wa leo ambao ni wa raundi ya nne ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kupambania kusepa na pointi tatu mwisho wa dakika 90, Polisi Tanzania wakaibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Marcel Kaheza alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 11 kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 uliozama moja kwa moja ndani ya lango lililokuwa chini ya Aron Kalambo.
Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika, Dodoma FC ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 kisha kipindi cha pili Polisi Tanzania waliongeza mabao mawili ambapo ilikuwa n kupitia kwa Tariq Seif aliyepachika bao hilo dakika ya 38 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Kaheza tena dakika ya 61.
Ushindi huo ni wa pili kwa Polisi Tanzania baada ya kushinda mechi yao ya kwanza mbele ya Namungo FC kisha leo inashinda mara ya pili mbele ya Dodoma FC ambayo nayo imepoteza kwa mara ya kwanza kwa kuwa ilikuwa imecheza mechi tatu bila kupoteza kwa msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment