September 13, 2020


 KLABU ya KMC imeendeleza moto wake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuinyoosha mabao 2-1 wapinzani wa Tanzania Prisons, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Septemba 12 Uwanja wa Uhuru.

KMC ilianza kuinyoosha Mbeya City kwa mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru, Septemba 7 ikiwa imeweka rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 kwenye mchezo mmoja mpaka sasa.

Hassan Kabunda alipachika bao la kwanza dakika ya 6 na lile la pili lilipachikwa na Kenetth Masumbuko huku lile la Tanzania Prisons likifungwa na Kassim Mdoe dakika ya 39.

Kazi inayofuata kwa KMC ambayo kwa sasa ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi sita na mabao sita ni Septemba 21 itakwenda kukutana na timu ya Mwadui ya Mkoani Shinyanga.

 Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo kamili kuendelea na mapambano kikubwa mashabiki waendelee kuwapa sapoti.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic