KOCHA Mkuu wa Aigle Noir ya Burundi, Gustave Niyonkuru, amevutiwa na kiwango kilichooneshwa na kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mkongomani, Tuisila Kisinda.
Kisinda ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Klabu ya AS Vita, amekuwa na kasi ndani ya uwanja huku wengi wakimtabiria kufanya makubwa msimu huu.
Kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, Kisinda alipachika bao moja wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 mbele ya timu hiyo Uwanja wa Mkapa.
Niyonkuru amesema:“Nimevutiwa na yule aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni na kufanikiwa kufunga bao la kwanza, wanamwita Kisinda, ni mchezaji mzuri na kwa kweli atawasaidia sana Yanga."
Kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Kisinda aliweza kufanya majaribio hatari matatu ambayo hayakuzaa matunda.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Septemba 6, Yanga ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na bao la Yanga lilipachikwa na Michael Sarpong.
Bado habari za Wiki ya Wananchi zinaendelea kuandikwa!?
ReplyDeleteUlitaka waandike wiki ya nani?
DeleteWiki ya mabeberu
DeleteVyura wamekosa habari
ReplyDeleteushabiki uliopindukia
ReplyDeletecarpets for living room
ReplyDeletejute mat
full room carpet
sisal carpet
round jute rug
jute flooring
seagrass carpet
jute mats
sisal rugs
jute rugs online india
online carpet
carpet living room
chindi rugs
jute carpets online india
jute carpet price
india rag
chindi
jute carpet
waste cloth craft
cotton carpet
Mwandishi acha mbwembwe wewe.
ReplyDelete