UONGOZI wa Dodoma Jiji FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara umesema kuwa malengo yao makubwa ni kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2020/21 hivyo watapambana kushinda kwenye mechi zao zote watakazocheza.
Leo Dodoma Jiji itakuwa kibaruani muda mfupi kuanzia sasa mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 8:00 mchana ni wa mzunguko wa nne ndani ya ligi.
Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Johnson Fourtnatus amesema: “Mikakati yetu ni kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo kwa msimu huu hivyo kila mchezo kwetu ni fainali kwa maana hiyo tutaingia uwanjani tukiwa tunajua tunaenda kupambana na timu nzuri.
"Pia lengo lengo letu ni kuona kwamba tunafanikiwa kuchukua ubingwa basi hawa wapinzani wetu leo hatutawaonea huruma.”
0 COMMENTS:
Post a Comment