September 12, 2020

 


MSHAMBULIAJI namba moja ndani ya Klabu ya Liverpool,  Mohamed Salah raia wa Misri leo amefunga hat trick ya kwanza ndani ya msimu mpya wa Ligi Kuu England wakati timu yake ikisepa na pointi tatu mazima mbele ya Leeds United. 


Mabao ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England yalipachikwa dakika ya 4 na mfunguzi akiwa Salah mwenyewe lilisawazishwa dakika ya 12 na Jack Harrison.


Iliwachukua Liverpool dakika 8 kupachika bao la pili kupitia kwa Virgil van Dijk dakika ya 20 lilidumu dakika 10 lilisawazishwa na Patrick Bamford dakika ya 30.


Salah alirejea kambani dakika ya 33 na kuwafanya Liverpool kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-2 ila dakika ya 66 Meteusz Klich wa Leeds United alisawazisha kabla ya Salah kupachika bao la tatu dakika ya 88 kwa mkwaju wa penalti.


Ni mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ikiwa msimu wa 2020/21  ndo kwanza unaanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic