September 22, 2020



OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amefichua kuwa kabla ya matokeo ya sare na Simba, wapinzani wao walijuwa watawafunga zaidi ya mabao 10 kutokana na uwepo wa wachezaji waliowasajili kwa gharama akiwemo Bernard Morrison na Larry Bwalya.

Kifaru ameongeza kuwa kwa aina ya wachezaji ambao Simba wamewasajili kwa gharama kubwa wengi walijuwa wangepoteza mechi hiyo na Simba kwa idadi kubwa ya mabao.

Mtibwa wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri, Morogoro waliwalazimisha Simba sare ya kufungana bao 1-1 ilikuwa ni Septemba 12.

Kifaru amesema kuwa: "Simba wamesajili kwa gharama kubwa sana, wengi walidhani kwamba watakuwa na uwezo wa kutufunga mabao mengi hata 10.
"Lakini wameona kuwa hizo fedha wangeweza kuwapa tu wachezaji wa hapa ndani kisha wakaifanya kazi yao vizuri kama ambavyo sisi tumefanya na kupata matokeo dhidi yao," aliweka nukta Kifaru.

Bao la Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin huku lile la Mtibwa Sugar likiwekwa kimiani na nyota wao Boban Zirintusa na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

8 COMMENTS:

  1. Ni simba Tu wanapewa somo sio Yanga kmc au azam

    ReplyDelete
  2. Hao mtibwa wanaosajili wachezaji wa ndani si waliponea chupuchupu kushuka daraja sasa somo gani anatoa au anaongea ili ajulikane yupo

    ReplyDelete
  3. Kifaru amesahau jinsi alivyokua akiwaomba hadi waandishi wa habari wawaombee ili wasishuke daraja. Leo eti anajifanya kutoa ushauri kwa Simba kuhusu usajili wa wachezaji. Aibu kweli kweli

    ReplyDelete
  4. Wenzio Kila siku wanapambana kuchukua ubingwa! wewe je unagombania nini au ndiyo nyege za mdomo zina kuwasha? tambua mchezaji bora wa mechi yenu kilikuwa (KIWANJA)chenu kizuri

    ReplyDelete
  5. Ofisa wa habari alichoeleza ni pumba tupu.Nina wasiwasi na cheti chake cha uandishi/utangazaji.Jitafakari

    ReplyDelete
  6. Licha ya Morogoro kuwa na hazina kubwa ya vipaji vya mpira lakini mkoa mzima miaka nenda miaka rudi wanashindwa kuwa na kiwanja chenye hazi ya ligi kuu mnapitwa na gwambina au yule kijana mdogo wa kitanzania aliejenga kiwanja chake binafsi kwa kweli morogoro kwa suala la uwanja mnajidhalilisha na kulidhalilisha taifa kwani morogoro ina thamani kubwa kwenye soka la Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Mtibwa pambaneni msishuke daraja, hamna somo lakumfundisha baa yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic