September 27, 2020

  


NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Obrey Chirwa amesema  kuwa ataendelea kujituma ili aendelee kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Zambia, 'Chipolopolo' kwa mara nyingine.

 

Staa huyo wa Azam ameitwa kwenye kikosi cha Chipolopolo kwa ajili ya mechi za timu hiyo ambazo watacheza dhidi ya Congo Oktoba 7, Kenya Oktoba 11 na Afrika Kusini Oktoba 13.

 

Chirwa amesema kuwa, kwake ni jambo zuri ambapo ataendeleza moto wake katika Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kupata nafasi ya kuitwa tena kwa mara nyingine.

 

“Najisikia vizuri, muda mrefu sijacheza timu ya taifa nilicheza chini ya miaka 20 na 23, najisikia furaha sana.

 

"Hii ni mara ya kwanza kuitwa timu hiyo ya wakubwa.Kuhusu mechi hizo, siyo ndogo kwa sababu hadi unaitwa timu ya taifa ni kuonyesha umeaminiwa na lazima uonyeshe kwenye timu ya taifa kwa sababu hata klabu yangu itakuwa inaniangalia.

 

“Nitaendelea kufunga na kuasisti mara kwa mara kwa ajili ya kunifanya niitwe katika timu ya taifa kila mara,” alimaliza Chirwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic