September 26, 2020


NYOTA wa Tanzania, Mbwana Samatta muda mfupi baada ya kuibukia ndani ya Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo akitokea Klabu ya Aston Villa ameanza kupiga matizi na wachezaji wenzake ndai ya kikosi chake kipya.

Samatta ameandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England na kufunga bao pia baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Alisaini dili la miaka minne ndani ya Astov Villa ambayo iliponea chupuchupu kushuka daraja kwa msimu wa 2019/20.


Klabu ya Aston Villa imemuaga nyota huyo kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya.


Mchezaji huyo aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.


Samatta amesema kuwa anafurahia maisha yake mapya na anawashukuru Aston Villa kwa kumpa nafasi ya kucheza kwenye ligi ya ndoto yake.

1 COMMENTS:

  1. Maneno ya kimpira hayo, siyo baadhi ya viazi vikitoka team mmoja kwenda nyingine vinazungumzia alikotoka vibaya. Mfano niyonzima.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic