September 26, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Mtibwa Sugar itakayopigwa Uwanja wa Jamhuri. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema kuwa, Kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic ameonekana kufurahishwa na kikosi chake ambacho kinampa matumaini ya kufanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yao.

 

“Kocha amefurahishwa na kikosi kutokana na vijana kuonekana kuimarika siku hadi siku.Tupo vizuri na tunaamini kwamba mechi zetu zote tutapata matokeo chanya.

 

“Sasa timu inaonekana kuwa imara baada ya kikosi kuzoeana hasa katika safu ya ushambuliaji, ni matumani yetu tutafanya vizuri zaidi katika mechi yetu dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi nyingine zinazofuata.

 

“Tunahitaji kujipanga kama unavyojua msimu huu tumejipanga tangu awali na tumekuwa vizuri, kufikisha pointi saba si kazi ndogo kama unavyoona wenye pointi tisa na saba ni timu chache hivyo unaona ni jinsi gani tulivyopambana,” amesema Mwakalebela.


Timu zote zinashuka uwanjani zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za hivi karibuni za ligi.


Yanga wenyewe wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Ihefu FC.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic