NYOTA wa Chelsea, Tammy Abraham aliokoa jahazi la Chelsea lisizame mbele ya West Brom kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.
Chelsea ilikuwa imebanwa mbavu na West Brom, Uwanja wa The Hawthorns wakati wakigawana pointi mojamoja.
Mabao ya wenyeji West Brom yalipachikwa kimiani na Callum Robinson aliyekuwa mwiba dk ya 4 na 25 na lile la tatu lilipachikwa na Kyle Bartley dk 27.
Chelsea wao walipata mabao kupitia kwa Mason Mount dk 55, Callum Hudson dk 70 na Abraham dk 90+3.
0 COMMENTS:
Post a Comment