September 27, 2020


 OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa timu yake kwa sasa haina uhitaji mkubwa wa kupata beki kwa kuwa anaamini wachezaji alionao ni imara na wanaweza kumpa mafanikio.


Kwa sasa Solskjaer yupo kwenye presha kubwa hasa baada ya kufungua pazia la Ligi Kuu England kwa kupokea kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Crystal Palace kabla ya jana kushinda kwa mbinde mabao 3-2 mbele ya Brighton mchezo uliochezwa Uwanja wa Falmer.

Mabao ya Brighton yalifungwa na Neal Maupay dk ya 40 kwa penalti na Solly March dk ya 90+4 huku yale ya United yakifungwa na Lewis Dunk dk 43 aliyejifunga, Marcus Rashford dk 55 na lile la ushindi lilifungwa na Bruno Fernandes dk 90+10 kwa penalti.

United imemuongeza nyota mmoja kikosini ambaye ni kiungo Donny van de Beek huku maswali mengi yakiwa ni kuhusu pacha ya mabeki kati ya Harry Maguire na Victor Lindelof itapatikanaje huku Solskjaer akisema kuwa haitaji saini ya beki .

"Kwangu mimi ninaona kwamba tuna safu imara ya mabeki kwa muda huu kilichoshindikana ni muundo pekee, muundo ukiwa mzuri basi tutafanya vema. Makosa ya mtu binafsi ni madogo sana," amesema Solskjaer.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic