KLABU ya Atletico Madrid imeripotiwa kuwa kwa siku za karibuni, haina mpango wa kufanya biashara tena na Arsenal kutokana na kilichotokea kwenye usajili wa Thomas Partey.
Partey amesajiliwa na Arsenal siku ya mwisho kabla ya usajili haujafungwa Jumatatu ya wiki hii ambapo uhamisho wake umegharimu pauni 45m.
Atletico wanadai kwamba, kitendo cha Arsenal kuchelewa kufanya mazungumzo na klabu hiyo huku ikizungumza zaidi na mchezaji kwa kumshawishi na mwisho wa siku kumsajili, ndiyo kimewaudhi kwa sababu imeshindwa kupata muda wa kumtafuta mbadala wake.
Ripoti kutoka Hispania zinadai kuwa, ombi la Arsenal kumuhitaji kiungo huyo lilifika dakika 32 kabla ya usajili kufungwa.
Jambo hilo liliwapa wakati mgumu mabosi wa Atletico kuweza kumpata mbadala wake kwa muda huo ambao ulikuwa umekwenda.
Partey akiwa Arsenal, atakuwa analipwa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki, huku mkataba wake ukiwa ni wa miaka minne.
0 COMMENTS:
Post a Comment