KUFUATIA Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kusogeza mbele mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ‘Kariakoo Dabi’ kumesababisha kumchelewesha kocha mpya wa Yanga, Cedric Kaze ambaye alitakiwa kutua jana Alhamisi, sasa atatua kesho leo Jumamosi au Alhamisi ijayo.
Simba na Yanga zilikuwa zikutane Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ambapo kwa sasa zitakutana Novemba 7 kutokana na sababu ya changamoto ambazo zimetajwa ni kuhusu tahadhari ya Corona kwa wachezaji wa kimataifa.
Yanga imeshamalizana na Kaze ambaye anakuja kubebe mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic tayari kwa ajili ya kuanza kukinoa kikosi hicho baada ya kutanguliza majembe yake ya ushindi.
Taarifa kutoka katika benchi la ufundi la Yanga zinasema kuwa, Kaze anatarajia kutua rasmi kuanza kuitumikia timu hiyo Alhamisi ijayo huku akiwa anaweka mipango yake sawa kabla ya kutua klabuni hapo.
“Awali alikuwa atue Alhamisi hii ili kujiandaa na mchezo wa Simba, ilikuwa lazima awahi kujiandaa na mchezo huo muhimu.
“Hivyo, baada ya kuahirishwa kwa mechi hiyo, sasa anamalizia mipango yake ili akija awe kamili kuanza kazi ya kuitumikia Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.
Pamoja na ripoti hiyo, taarifa nyingine zilieleza kuwa kocha huyo anaweza kuingia Dar, leo Jumamosi kama baadhi ya mambo yataenda sawa kama ambavyo mwenyewe amekuwa akipanga.
kwa hiyo muunganiko wenu hautaathirika wazee wa chemistry?
ReplyDeletekama taarifa hii inatoka kwa viongoz basi jueni mnaferi sana.
ReplyDeletekwann waongo kias hicho, au mnafikir mnaongoza watoto wenu.
kuweni wa kweli.
timu haielewek inatumia mfumo gani, wachezaj hawana fiziki watu ufund, mechi mnashinda kibahati tu, kkn mnakuja kusema kocha anamalizia mambo yake, kisa mech imesogezwa mbele.
baadae mnakuja kusema simba ananunua mechi, mara anahonga waamuz,
mm ni shabiki wa yanga lkn ktk hili siwaamini viongoz wangu.
huu muda ndio ilikjwa bahat kwetu kocha akuje mapema aweke sawa wachezaji, kama tatizo tiket waambieni wananchi sio kuleta siasa
wewe ni mamluki cio shabiki wa yangu wew
DeleteInawezekana kabisa uwezo wa mdhamini kifedha haupo vizuri, ndio maana walileta wachezaji huru " free agent" Michael sarpong, Sogne, Carlnos nk na pia juma mwambusi alikuwa huru pamoja na zlatco wote walikuwa huru, walimshindwa mexime kwasababu hawakuwa na hela aliyotaka, walimshindwa Bwalya na Mugalu tatizo ni hela, wanamtaka Kaze lakini wanashindwana kwenye hela, kumtoa mbongo Canada umrudishe east africa ina kupasa umthibitishie uhakika wa kumlipa hela aitakayo. Tatizo la Yanga ni hela, mauzo ya Jezi ni mpango wa kupata kipato cha kuendesha timu nk, tatizo matumizi yamezidi mapato na timu inayumba, watu wenyewe hawashauriki wamegeuka kuwa wanasiasa wa mpira.
ReplyDeleteUmejitahidi kuwajua Yanga wasaidie basi
ReplyDeleteClub haina pesa wape the way foward,na je Mo kalipa 20b au anakata mumo mumo kwenye matumizi.
ReplyDeleteumeshawai kusikia timu inayumba hata kama hajaweka 20 bilioni ambazo na sisi hatutaki aweke ila cha msingi atuletee majembe ya maana Afrka kama Larry Bwalya na Luis na mchezaji bora kuliko wote waliopo Afrika Mashariki Triple C
DeleteAchana naye hyo utopolo anamawazo ya kimaskini, zile bikini 20 nikwaajili ya uemwekezaji sehemu mbalimbali ziweze kuzalisga nyingine zaidi. Mfano tunatia 10 milioni tunawekeza Voda, 5 milioni tunawekeza tiga cement, 20 milioni tunawekeza NMB hivyo mpaka mwisho. Kika mwezi Simba itakuwa insvuna kwenye hayo makampuni iliyowekeza mikwanja nakufanya team kuendelea kukua kiuchumi. Tatizo wengi wao utopolo hawana elimu ya kimaendeleo.
ReplyDeleteSorry bilioni 20 cyo bikini nimakosa ya uandishi
ReplyDeleteMo bdo anaunda uongozi vzr nakuweka sawa atie mkwanja lengo kila kitu kiende sawasawa bila makumbano. Simba nguvu moja
ReplyDelete