October 13, 2020

 


OKTOBA 15, Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba mwenye tuzo ya kocha bora Septemba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Mwadui FC inayonolewa na Khalid Adam.


Kwa sasa Azam FC ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 5 na hawajapoteza mchezo mpaka sasa.


Jambo hilo lilimfanya Cioaba na nyota wake chaguo la Kwanza Prince Dube kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba baada ya kufunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao.


Ndani ya mwezi Oktoba tayari amefunga mabao mawili na kumfanya afikishe jumla ya mabao matano akiwa ni kinara wa kutupia ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Azam FC mchezo wake wa mwisho raundi ya tano ilishinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex inakutana na Mwadui FC ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Majaliwa.


Cioaba amesema kuwa anaamini vijana wake watapambana kupata matokeo chanya uwanjani ili kuendeleza rekodi nzuri.


Adam wa Mwadui amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ushindani na amewambia waongeze umakini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic