NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo (35) amebainika kuwa ameambukizwa Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19. Benchi la ufundi la mabingwa hao wa Ulaya limethibitisha taarifa hiyo.
Ronaldo ambaye pia ni mshambuliaji wa Klabu ya Juventus ya Italia, ataukosa mchezo muhimu wa kundi C kesho kati ya Ureno dhidi ya Sweden, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Avalade, katika mbio za kuwania kufuzu mashindano ya Uefa Nation League.
Tayari amesharuhusiwa kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo akiwa ni mchezaji pekee aliyeambukizwa virusi hivyo lakini hajaonyesha dalili zozote za Covid 19.
Ronaldo ni staa wa kwanza kupatikana na Corona hivi karibuni. Wachezaji wenzake wa Juventus, Blaise Matuidi, Paulo Dybala na Daniele Rugani walikutwa na Corona miezi michache iliyopita.
Wengine ni Thiago Alcantara, Aymeric Laporte na Riyad Mahrez.
0 COMMENTS:
Post a Comment