October 27, 2020

 




UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar halikuwa fungu lao la kupata ndio maana wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Azam FC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ilikuwa imecheza jumla ya mechi saba bila kupoteza ilipoteza mchezo wake wa kwanza jana, Oktoba 26, Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kufungwa na Mtibwa Sugar.

Bao pekee la ushindi lililowapoteza Azam FC lilipachikwa na mbaya, Jaffay Kibaya dakika ya 62 na kudumu mpaka dakika ya 90 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:-"Wachezaji wamefanya kazi nzuri mwisho wa siku matokeo hayakuwa upande wetu. Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza kwa msimu wa 2020/21.

"Bado ni sehemu ya mchezo na tutaendelea kupambana kwani haikuwa fungu letu la kushinda tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo, tuna kikosi kizuri na wachezaji wapo vizuri."

Kwenye mchezo wa jana ni nyota wawili wa kikosi cha kwanza walikosekana ambao ni Obrey Chirwa abaye ni mshambuliaji mwenye mabao manne alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya enka.

Salum Abubakar, Sure Boy alikuwa ana adhabu ya kadi tatu za njano, yeye ana pasi moja ya bao.

Azam FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi nane, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 11 nayo imecheza mechi nane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic