KOCHA Mkuu
wa Mbao, Salmin Kamau, ameachia ngazi huku akidai timu yake inapitia katika
mazingira magumu na uongozi usipochukua hatua za haraka lolote linaweza
kutokea.
Kocha huyo
alitoa rai hiyo mara baada ya kumalizika kwa 'dabi' ya Mwanza na timu yake
kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Pamba, katika mchezo uliopigwa Dimba
la CCM Kirumba Oktoba 24.
Dalili za
Pamba kushinda mchezo zilianza mapema kwani dakika ya sita ya mchezo ilitosha
kuwapatia bao la kuongoza kupitia kwa Shaaban Imamu, kabla ya kurudi tena
nyavuni na kuwapatia bao la pili dakika 40 ya mchezo na bao la tatu
likihitimishwa na Ajib Mohamed dakika ya 76.
Kamau alisema
kwanza anawapongeza wachezaji wake wamepambana vya kutosha kwani timu yake
walikutana saa 8 mchana masaa mawili kabla ya mchezo, akiwa hafahamu kama
mchezaji kaja ana tatizo gani, je amekula na kushiba, sasa kwa mazingira hayo
ndiyo maana anasema wamejitahidi sana.
"Kikuweli
Mbao tuna mazingira magumu sana na mimi kama kocha nashindwa kutekeleza majukumu
kwa wachezaji wangu kwani mazingira ninayoyaona timu haina kambi, mchezaji
anatoka kwao saa 1 kabla ya mchezo umempimaje kujua kama yupo fiti kwa ajili ya
mchezo husika na haya ndo matokeo tunayopata, kama hatutakuwa makini lolote
linaweza kutokea, " alisema kocha huyo.
Hata hivyo,
baadaye taarifa zilitokea kuwa kocha huyo ameamua kuachia ngazi ambapo
alipoulizwa alisema: “Ni kweli nimekaa na kutafakari na sasa nimeamua kujiuzulu
nafasi yangu ya ukocha katika timu ya Mbao na sababu kubwa ni kutokana na timu
yetu kukabiliwa na ukata kiasi kwamba timu inashindwa kujihudumia yenyewe.”
0 COMMENTS:
Post a Comment