BAADA ya kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye ligi kuu msimu huu, kikosi cha Mbeya City kimetamba kuibuka na ushindi kwenye michezo iliyoko mbele yao.
Mwishoni mwa
wiki iliyopita, Mbeya City walifanikiwa kupata ushindi wa kwanza msimu huu
ambapo walifanikiwa kuifunga Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani
Kagera.
Mpaka sasa
Wagonganyundo hao wa Jiji la Mbeya, wamefanikiwa kujikusanyia pointi tano baada
ya kucheza michezo nane.
Kocha
Msaidizi wa Mbeya City, Mathias Wandiba alisema sasa wanajiandaa na mchezo ujao
dhidi ya Ihefu.
"Tunamshukuru
Mungu tumefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye ligi na tunaamini huu ndiyo
mwanzo wetu kwenye ligi," alisema kocha huyo.
Mchezo wao
ujao unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mwishoni mwa
wiki hii.
Mbeya City ilimfuta kazi kocha wake Amri Said ambaye kutokana na mwendo wake kuwa wa kususua ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment